Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania, Salum Mayanga (pichani) leo
Ijumaa Machi 19, 2017 ametangaza majina ya wachezaji 24 watakaounda
kikosi hicho cha Timu ya Taifa Stars ambacho sasa kinachodhaminiwa na Kampuni
ya Bia ya Serengeti.
Katika mkutano na wanahabari uliofanyika Makao Makuu ya
TFF, yaliyoko Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam, Mayanga alisema
kikosi hicho kinaundwa na makipa Aishi Manula (Azam FC), Benno Kakolanya
(Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).
Walinzi wa pembeni upande wa kulia aliwataja Shomari
Kapombe (Azam FC) na Hassan Kessy (Yanga SC) wakati upande wa
kushoto wapo Mohammed Hussein (Simba) na Haji Mwinyi (Yanga SC).
Mayanga aliwataja walinzi wa kati Erasto Nyoni
(Azam FC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Aggrey Morris
(Azam FC) ilihali aliwataja viungo wa kuzuia kuwa ni Himid Mao (Azam FC)
na Jonas Mkude (Simba SC).
Kadhalika wako viungo wa kushambulia Salum Abubakar
(Azam FC), Said Ndemla (Simba SC) na Muzamiru Yassin (Simba) wakati
viungo wa kulia waliotajwa ni Simon Msuva (Yanga SC) na Shizza Kichuya (Simba
SC).
Viungo wa kushoto ni Farid Mussa (Teneriffe,
Hispania) wakati washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk- Ubelgiji),
Thomas Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden), Ibrahim Ajib (Simba SC), Mbaraka
Yusufu (Kagera Sugar) na Abdurahman Mussa (Ruvu Shooting).
Pia Mayanga aliwataja wasaidizi wake kuwa ni Kocha
Msaidizi kuwa ni Novatus Fulgence wakati Kocha wa Makipa, Patrick
Mwangata wakati Meneja wa atakuwa Danny Msangi; Mtunza Vifaa, Ally Ruvu wakati
Daktari wa timu atakuwa Richard Yomba huku Daktari wa viungo akiwa
ni Gilbert Kigadya.
Timu hiyo itaingia kambini Machi 23, 2017 kwenye Hoteli
ya Urban Rose, Dar es Salaam mpaka tarehe 29 baada ya hapo itasafiri kwenda
Misri kwa kambi ya wiki moja kabla ya kurejea kuja kucheza mchezo wa kufuzu
Mataifa huru ya Afrika mchezo na Lesotho, mchezo utachezwa Tarehe 10
mwezi wa 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...