Na Karama Kenyuko, Globu ya Jamii

Wafanyabiashara wa kemikali Bashirifu wameaswa kufuata sheria za nchi Katika kudhibiti matumizi yasiyokuwa salama ya kemikali hizo.

Hayo yamesemwa Leo na Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya kampuni ya Tecno Net Scientific kukutwa na Kemikali Bashirifu bila ya kuwa na kibali wala usajili.

Profesa Manyele amesema, mwaka 2014 waliipatia kampuni hiyo usajili wa miaka miwili, lakini baada ya kibali chao kuisha wamekiuka sheria na kuendelea kuagiza Kemikali bashirifu kwa kutumia vibali bandia.

Ameongeza kuwa, kufuatia kugundua hayo, vyombo vya dola vinafanya uchunguzi wa shughuli za kampuni hiyo na pindi taratibu za uchunguzi utakapokamilika kampuni hiyo itafikishwa mahakamani.

Aidha ameongeza kuwa, ili kuhakikisha kemikali hizo zinatumika katika hali iliyosalama, wafanyabiashara wote wanaojihusisha na Kemikali, kudhibiti matumizi matumizi yasiyofaa na kuzuia kutumia kwa kutengeneza mabomu, milipiko dawa za kulevya au kutumia kama silaha kama ilivyokuwa kwenye suala la watu kumwagiwa tindikali.

Aidha Prof. Manyele amesema, wafanyabiashara wote wanaojihusisha na biashara ya Kemikali bashirifu kuhakikisha wanaenda Kutoa taarifa mwenyewe pindi vibali vyao vikiisha ili wapatiwe usajili mpya.Amesema, Serikali haitasita kuwachukulia hatua wafanyabiashara wa kemikali wasiokuwa waaminifu na wanaovunja matakwa ya sheria katika uingizaji na usafirishaji wa Kemikali bashirifu.

Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyere akizungumza na waandishi habari juu uingizaji Kemikali bashirifu ambazo zinafuata sheria iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...