RAIS Dk John Pombe Magufuli anaendelea kutekeleza kwa kasi ahadi zake alizowaahidi wananchi wa Tanzania wakati akiwaomba kura wakati wa kampeni mwaka 2015.

Katika mkoa wa Kigoma moja ya ahadi zake kwa wananchi wa Mji mdogo wa Nguruka wilayani Uvinza, Rais Magufuli aliwaahidi wananchi hao kuwa ataitatua shida ya maji ya muda mrefu inayowakabili.

Rais Magufuli aliwahakikishia wananchi hao kuwa kupitia mto Malagarasi ambao ni jirani tu na mji huo (Kilomita 18 kutoka mji wa Nguruka) atawajengea mradi mkubwa wa maji ambayo yatatumika katika Wilaya yote ya Uvinza na maeneo jirani.

Hatimaye leo Rais Magufuli ameitekeleza ahadi yake na kuweka jiwe la msingi la mradi huo mkubwa kabisa katika miradi iliyopo mkoani Kigoma. Kwamujibu wa Rais Magufuli mradi huo utakamilika Desemba 31, 2017 na kuanza kuwahudumia wananchi ambao wana hamu kubwa ya kuona mradi huo ukianza kuwapatia maji.

Hizi ni juhudi za Rais za kuhakikisha kuwa wananchi wa Tanzania wanafaidika na rasilimali za nchi yao ambapo amefanikiwa kulinda rasilimali za nchi na kupambana bila kuchoka na wabadhirifu wa mali za umma, wala rushwa na mafisadi.

Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wananchi wa Nguruka Uvinza Mkoani Kigoma,wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Tanki la Kuhifadhia Maji kwaajili ya Wananchi wa Nguruka. Julai 23,2017.

Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia Wananchi mbalimbali wa mji wa Nguruka mapema leo asubuhi,waliojitokeza kumshuhudia Rais akiweka jiwe la msingi la Mradi wa maji.Rais Magufuli ametekeleza ahadi yake ya kuupatia maji mji wa Nguruka Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma,ambapo pia ameweka jiwe la msingi la mradi huo unaotarajia kukamilika Desemba 31, 2017,ukamilishwaji wa mradi huo utamaliza tatizo la maji la Mji wa Nguruka.

Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipeana mkono na Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge mara bada ya kuweka jiwe la msingi la maradi wa maji Nguruka. Julai 23,2017.
 Rais Dkt Magufuli akipeana mkono na Mbunge wa jimbo la Kasulu Mjini,Mh Daniel Nsanzugwako mara baada ya kuweka jiwe la msingi la Mradi mkubwa wa maji mapema leo mjini Nguruka mkoni Kigoma.Rais Magufuli ametekeleza ahadi yake ya kuupatia maji mji wa Nguruka Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma,na kuwamba Mradi huo unatarajia kukamilika Desemba 31,2017,kukamilika kwa mradi huo utamaliza tatizo la maji la Mji wa Nguruka.
 Rais Dkt Magufuli akitoka kukagua mradi huo wa maji unaotarajia kukamilika Desemba 31,2017.kukamilika kwa mradi huo utamaliza tatizo la maji la Mji wa Nguruka.Rais Dkt Magufuli yuko njiani akielekea mkoani Tabora,ambapo atasimama Wilayani Kaliua na kuzindua barabara ya Kaliua hadi Kazilambwa yenye urefu wa kilometa 56.

Rais wa Jamuhuri Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwasalimia Mamia ya Wananchi wa Nguruka Uvinza Mkoani Kigoma mara baada ya kuhitimisha kuwahutubia wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Tanki la Kuhifadhia Maji kwaajili ya Wananchi wa Nguruka Julai 23,2017.


Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...