Na Evelyn Mkokoi – Dar Es Salaam.
Garage
kubwa yenye kutoa huduma kwa magari ya aina mbalimbali iliyopo katika
eneo la mtaa wa viwanda mikocheni jijini Dar es Salaam imefungwa kwa
kile kinachodaiwa ni kukikuka sheria ya mazingira na kanuni zake kwa
kuharibu mazingira kwa kumwaga mafuta machafu, kutupa vyuma chakavu na
kutelekeza magari yaliyochoka.
Hatua
Hiyo imechukuliwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira (NEMC) kupitia Afisa Sheria Mkuu wake Bw. Vincent Haule,
ambapo Bwana Haule Alisema kuwa Garage Hiyo ambayo Mmiliki wake
hakutambulika Mara moja inatakiwa kusimamisha shughuli zote za
uendeshaji katika eneo hilo ndani ya siku saba pamoja na kuondoa magari
yote.
Bw.
Haule aliongeza kwa kusema kuwa Mmiliki wa Garage hiyo anatakiwa
kufuata taratibu za serikali kwa kupata vibali vyote vya uendeshaji
ikiwa ni pamoja na kibali maalum kutoka NEMC.Baada ya kutozwa faini ya
shilingi milioni 10 kwa kiwanda cha Bidco kinachotengeneza bidhaa za
sabuni na mafuta ya kula na kutakiwa kuilipa faini hiyo ndani ya wiki
mbili, Naibu Waziri Ofisi ya Makami wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.
Luhaga Mpina, alisema viwanda vinavyochukuliwa hatua kwa uchafuzi wa
mazingira vinatakiwa kutii maagizo ya serikali.
Mpina
pia alitoa maelekezo kwa Manisapaa ya Kinondoni ambapo aliitaka
ishughulikie mitaro katika maeneo ya mikocheni pembezoni mwa viwanda
husika na kuondosha maji katika njia sahihi.Kwa upande wa wenye viwanda,
Mpina aliwata kuacha kutiririsha majitaka katika mazingira na kuyatibu
na kuyaunga katika mfumo sahihi wa uondoshwaji maji hayo wa DAWASCO ili
kunususru uharibifu wa mazingira na afya ya viumbe hai.
Aidha,
Mpina aliwataka wamiliki wa kiwanda cha Bidco kuendelea kutoa
ushirikiano kwa kuziba matundu yanayotoa maji machafu kutoka kiwandani
hapo sambamba na kusafisha mitaro yote kiwandani humo. Ziara ya siku
mbili ya Naibu Waziri Mpina jijini Dar es Salaam ilihusisha Ukaguzi wa
Mazingira na Utekelezaji wa Sheria hiyo.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga
Mpina(kushoto) akimsikiliza mtaalam Bw. Filbert Mdonko, kutoka katika
kiwanda cha Intergraded Steel Limited kilichopo katika eneo la viwanda
Mikocheni Dar es Salaam namna ambavyo Mtambo wa kusafisha Majitaka
unavyofanya kazi.
Sehemu ya eneo la Garage iliyofungwa kwa uchafuzi wa mazingira katika eneo la viwanda Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano a Mazingira Mhe. Luhaga Mpina,
akiongea na kuonyesha maji machafu na yenye sumu yaliyotuwama na maji
hayo yanayotoka viwandani katika eneo la Mikocheni Jijini Dar es Salaam
alipoendelea na ziara yake ya ukaguzi wa viwanda na utekelezaji wa
Sheria ya Mazingira leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...