Na Tiganya Vincent.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amefanikiwa kumaliza mgogoro kati ya waliokuwa wafanyakazi 11 wa Kampuni ya Ujenzi ya Ceytun iliyokuwa ikipanua Uwanja wa Ndege wa Tabora na wamiliki wake juu ya kulipwa madai ya malipo ya muda wa ziada na mapunjo ya mishahara.

Mgogoro huo ulimalizika jana mjini Tabora baada ya Wamiliki wa Kampuni hiyo kukubali na kulipa madeni ya wafanyakazi wake ambapo  malipo yalifanyika mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Mkuu wa Wilaya ya Tabora.
Hatua hiyo ilifikiwa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kuamuru kuwang’anywa Hati za kusafiria za viongozi wake wawili wa Kampuni hiyo na kuzuiwa kwa vifaa vyake vya  ujenzi baada ya kuonekana kuwa anataka kuondoka bila kulipa malipo ya wafanyakazi hao.

Akizungumza mara baada ya Kampuni hiyo kuwalipa waliokuwa  wafanyakazi wake Mwanri alisema kuwa amelizika na kazi iliyofanyika na hivi sasa wanaweza kuchukua hati zao za kusafiria na wako huru kuondoa vifaa vyao vya ujenzi kwa sababu wamemalizana na watumishi hao bila kinyongo.

Aliomba Kampuni hiyo ikipata kazi nyingine isisite kuwapa ajira waliokuwa wafanyakazi wake licha ya mvutano uliotokea na kuongeza kuwa kilichotekea ndio mwanzo wa kuboresha mahusiano katika siku za baadaye.
Mwanri alisema kuwa uungwana waliouonyesha kukabali kukaa pamoja na kumaliza tofauti zao na waliokuwa wafanyakazi wao umeonyesha ni Kampuni inayostahili kuendelea kupewa kazi nyingine hapa nchini.

Aliwataka kutofunga milango kwani inawezekana wapo waliokuwa wafanyakazi wao ambao walisahaulika na wameshaondoka na pindi watakapokuja na vielelezo vinavyoonyesha kuwa bado wanadai basi wasaidiwe na walipwe haki zao.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...