Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo imeshindwa kuendelea kusikiliza ushahidi dhidi ya kesi ya kuzuia Jeshi la Polisi kufanya kazi yake, inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forum, Maxence Melo na mwanahisa wa mtandao huo, Mike Mushi kwa sababu shahidi alikuwa hajaandaliwa.

Aidha upande wa Mashtaka uliokuwa ukiongozwa na wakili wa serikali, Nassoro Katuga ulidai kuwa jalada la kesi hiyo lipo Polisi, na kwamba  mawakili wa serikal wanaosikiliza kesi hiyo wanamajukumu mengine ya kikazi katika mahakama tofauti.

Wakili Katuga amedai hayo yote mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

Hakimu Mwambapa ameahirisha kesi hiyo hadi October 17, 2017 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.

Katika kesi hiyo, Melo na mwenzake wanakabiliwa na kosa moja la kuzuia jeshi la polisi kufanya kazi yake.

Inadaiwa washtakiwa walitenda kosa hilo kati ya Aprili 1 na Desemba 13, mwaka jana katika maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...