Wakili marufu wa kujitegemea Dkt. Ringo Tenga (aliye mbele), akifuatiwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB), Peter Noni na wenzao wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, walipofikishwa kusomewa kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili. Kesi hiyo inatarajiwa kisikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa.
Wakili marufu wa kujitegemea Dkt. Ringo Tenga, aliyekuwa Mkurugenzi wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB), Peter Noni na wenzao wakiwa katika Ukumbi Wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakisubiri kusomewa kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili. Kesi hiyo inatarajiwa kisikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa.


Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii
Vigogo wanne wa Kampuni ya Six Telecoms Limited na kampuni yenyewe leo Novemba 20/ 2017 wamefikishwa  kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi likiwemo kuisababishia serikali hasara ya USD m.3.7 ambayo ni sawa na bilioni nane. Washtakiwa hao ambao walifikishwa mahakamani hapo majira ya saa tatu leo asubuhi wamesomewa mashtaka yao na wakili wa Serikali, Jehovaness Zacharia  mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Victoria Nongwa.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mhandisi  na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Hafidhi  Shamte, aliyekuwa Mkurugenzi wa benki ya Rasilimali watu (TIB),  Mfanyabiashara na pia ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Peter Noni, Wakili maarufu wa kujitegemea, Mhadhiri na Mkurugenzi pia wa kampuni hiyo Ringo Tenga,  Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo Noel Chacha na Kampuni ya Six Telecoms Limited. 

Akisoma hati ya mashtaka katika kesi hiyo namba 73 ya 2017, Wakili Zacharias alidai kuwa kati ya Januari Mosi 2014 na Januari 14, 2016 jijini Dar es Salaam washtakiwa hao, walitoza maalipo ya Mawasiliano ya simu za kimataifa chini ya kiwango  cha dola 0.25 kwa dakika kwa lengo la kujipatia faida binafsi.

Alidai kuwa katika siku hizo hizo washtakiwa kwa udanganyifu na kwania ya kuepuka maalipo, walishindwa kulipa kiasi cha dola 3,282,741.12 kama mapato kwa TCRA. Vile vile washtakiwa hao wanadaiwa kushindwa kulipa ada za udhibiti za dola 466,010.07 kwa TCRA.

Katika mashtaka ya utakatishaji washtakiwa Hafidhi, Noni,Tenga na Chacha wanadaiwa kujipatia, kutumia ama walisimamia USD 3,282,741.12 wakati wakijua fedha hizo ni zao la makosa ya udanganyifu linalotokana makosa mengine wanayoshtakiwa nayo.

Aidha katika shtaka la tano,  inadaiwa kuwa kampuni ya Six Telecoms  ilijipatia, ilitumia na kusimamia dola 3,282,741.12 wakati ikijua fedha hizo ni zao la makosa ya udanganyifu yanayotokana Mashtaka yaliyotangulia.

Katika shtaka la mwisho, washtakiwa wote hao waliisababishia TCRA hasara ya USD 3,748,751.22 ambayo ni sawa na bilioni nane za kitanzania. Washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu Mahakama ya Kisutu hiyo haina Mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

 Hata hivyo, baada ya kumaliza kusomwa kwa mashtaka dhidi ya washtakiwa, Wakili wa utetezi, Masumbuko Lamwai aliiomba Mahakama kukataa mashtaka dhidi ya washtakiwa na kuomba awaambie upande wa mashtaka wakaandae upya mashtaka na kuwaleta mahakani. Amesema mashtaka dhidi ya washtakiwa yameletwa haraka haraka na mashtaka hayako sawa sawa. Mashtaka haya hayaonyeshi mshtakiwa yupi katenda kosa gani, hati ya mashtaka ilitakiwa kuonyesha makosa.

Baada ya mabishano makali ya kisheria, mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Novemba 24, mwaka huu kwa ajili ya kutolea maamuzi mabishano hayo. Washtakiwa wamerudishwa rumande. upelelezi bado haujakamilika.
 
Wakili marufu wa kujitegemea Dkt. Ringo Tenga (aliye mbele), akifuatiwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB), Peter Noni wakipata kwenye basi la Magereza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...