Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeridhia na kupitisha jumla ya Shillingi Billioni 898 kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

Wakijibu hoja mbalimbali za wabunge kuhusu Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amesema Wizara itaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu Ukatili wa kijinsia ikiwemo kutoa elimu kwa wazazi ili wawafundishe watoto wao.

Pia Mhe. Ummy Mwalimu amesisitiza kuwa kwa somo la elimu ya uzazi kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ili kuwapa uelewa wanafunzi ili waweze kujikinga na kujiepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Serikali imefanya uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) nchini kwa kuyahakiki na kuyafuta Mashirika yote ambayo yamekosa sifa na kutofuata utaratibu na Sheria za nchi.

Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa Serikali inaendelea kutoa huduma kwa wazee nchini kwa kuboresha makazi ya kulea wazee wasiojiweza, kuanzisha na kuratibu madirisha maalum ya kutoa huduma za afya kwa wazee katika hospitali na kutoa kadi za matibabu kwa wazee hao. 

Bunge limepitisha Bajeti hii ikiwa imejumuisha fedha kwa ajili ya matumizi ya kawaida na matumizi kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...