THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MKUTANO MKUU WA KWANZA WA MWAKA WA WADAU WA MFUKO WA WCF KUFANYIKA NOVEMBA 29 - 30 2017 JIJINI ARUSHAMAHAFALI YA KUMI NA MBILI (12) YA CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE


MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT MAGUFULI AENDESHA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM

Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM na sekretarieti yake baada ya kikao jijini Dar es salaam leo Novemba 20, 2017.
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakiongea baada ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM jijini Dar es salaam leo Novemba 20, 2017.Picha na IKULU.


MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa kaongozana
 na Katibu Mkuu wake Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM  jijini 
Dar es salaam  leo Jumatatu Novemba 20, 2017
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akiwa kaongozana na Katibu Mkuu wa chama hicho  Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili katika kikao cha Kamati Kuu ya CCM  jijini Dar es salaam  leo Jumatatu Novemba 20, 2017
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli akiweka sawa makabrasha kabla ya kuanza kwa  kikao cha Kamati Kuu ya CCM  jijini Dar es salaam  leo Jumatatu Novemba 20, 2017

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt John Pombe Magufuli akiweka sawa makabrasha kabla ya kuanza kwa  kikao cha Kamati Kuu ya CCM  jijini Dar es salaam  leo Jumatatu Novemba 20, 2017


  Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)  Ndugu Abdulrahman Kinana akithibitisha kutimia kwa akidi kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM jijini Dar es salaam kinachoongozwa na Mwenyekiti wa
chama hicho Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumatatu Novemba 20, 2017.
MELI YA CHINA YAWASILI JIJINI DAR KUTOA HUDUMA ZA MATIBABU KUANZIA LEO JUMATATU HADI IJUMAA


BREAKING NYUZZZZ.....: WAKILI MAARUFU WA KUJITEGEMEA DKT. RINGO TENGA NA ALIYEKUWA MKURUGENZI MKUU WA TIB, PETER NONI WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA UHUJUMU UCHUMI

Wakili marufu wa kujitegemea Dkt. Ringo Tenga (aliye mbele), akifuatiwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB), Peter Noni na wenzao wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, walipofikishwa kusomewa kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili. Kesi hiyo inatarajiwa kisikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa.
Wakili marufu wa kujitegemea Dkt. Ringo Tenga, aliyekuwa Mkurugenzi wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB), Peter Noni na wenzao wakiwa katika Ukumbi Wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakisubiri kusomewa kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili. Kesi hiyo inatarajiwa kisikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa.


Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii
Vigogo wanne wa Kampuni ya Six Telecoms Limited na kampuni yenyewe leo Novemba 20/ 2017 wamefikishwa  kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi likiwemo kuisababishia serikali hasara ya USD m.3.7 ambayo ni sawa na bilioni nane. Washtakiwa hao ambao walifikishwa mahakamani hapo majira ya saa tatu leo asubuhi wamesomewa mashtaka yao na wakili wa Serikali, Jehovaness Zacharia  mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Victoria Nongwa.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mhandisi  na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Hafidhi  Shamte, aliyekuwa Mkurugenzi wa benki ya Rasilimali watu (TIB),  Mfanyabiashara na pia ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Peter Noni, Wakili maarufu wa kujitegemea, Mhadhiri na Mkurugenzi pia wa kampuni hiyo Ringo Tenga,  Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo Noel Chacha na Kampuni ya Six Telecoms Limited. 

Akisoma hati ya mashtaka katika kesi hiyo namba 73 ya 2017, Wakili Zacharias alidai kuwa kati ya Januari Mosi 2014 na Januari 14, 2016 jijini Dar es Salaam washtakiwa hao, walitoza maalipo ya Mawasiliano ya simu za kimataifa chini ya kiwango  cha dola 0.25 kwa dakika kwa lengo la kujipatia faida binafsi.

Alidai kuwa katika siku hizo hizo washtakiwa kwa udanganyifu na kwania ya kuepuka maalipo, walishindwa kulipa kiasi cha dola 3,282,741.12 kama mapato kwa TCRA. Vile vile washtakiwa hao wanadaiwa kushindwa kulipa ada za udhibiti za dola 466,010.07 kwa TCRA.

Katika mashtaka ya utakatishaji washtakiwa Hafidhi, Noni,Tenga na Chacha wanadaiwa kujipatia, kutumia ama walisimamia USD 3,282,741.12 wakati wakijua fedha hizo ni zao la makosa ya udanganyifu linalotokana makosa mengine wanayoshtakiwa nayo.

Aidha katika shtaka la tano,  inadaiwa kuwa kampuni ya Six Telecoms  ilijipatia, ilitumia na kusimamia dola 3,282,741.12 wakati ikijua fedha hizo ni zao la makosa ya udanganyifu yanayotokana Mashtaka yaliyotangulia.

Katika shtaka la mwisho, washtakiwa wote hao waliisababishia TCRA hasara ya USD 3,748,751.22 ambayo ni sawa na bilioni nane za kitanzania. Washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu Mahakama ya Kisutu hiyo haina Mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.

 Hata hivyo, baada ya kumaliza kusomwa kwa mashtaka dhidi ya washtakiwa, Wakili wa utetezi, Masumbuko Lamwai aliiomba Mahakama kukataa mashtaka dhidi ya washtakiwa na kuomba awaambie upande wa mashtaka wakaandae upya mashtaka na kuwaleta mahakani. Amesema mashtaka dhidi ya washtakiwa yameletwa haraka haraka na mashtaka hayako sawa sawa. Mashtaka haya hayaonyeshi mshtakiwa yupi katenda kosa gani, hati ya mashtaka ilitakiwa kuonyesha makosa.

Baada ya mabishano makali ya kisheria, mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Novemba 24, mwaka huu kwa ajili ya kutolea maamuzi mabishano hayo. Washtakiwa wamerudishwa rumande. upelelezi bado haujakamilika.
 
Wakili marufu wa kujitegemea Dkt. Ringo Tenga (aliye mbele), akifuatiwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB), Peter Noni wakipata kwenye basi la Magereza.


ASASI ZA KIRAIA ZAIOMBA SERIKALI KUBORESHA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI


Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Edda Sanga (kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani. Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Walemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Felician Mkude.

Mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani umeiomba Serikali kuifanyia maboresho sheria ya Usalama barabarabi ya mwaka 1973 ili iweze kukabiliana ipasavyo na suala la ajali za barabarani pamoja na athari zinazotokana na ajali hizo.

Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki  jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Edda Sanga alipokuwa akisoma tamko la pamoja la asasi hizo katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani.

“Pamoja na mambo mengine, katika kuadhimisha siku hii tunaisihi serikali na watunga sheria kuifanyia maboresho sheria ya Usalama barabarabi ya mwaka 1973 ili iweze kukabiliana ipasavyo na suala la ajali za barabarani pamoja na athari zinazotokana na ajali hizo,” alisema Bi. Sanga.

Alisema miongoni mwa maeneo wanaoshauri marekebisho/maboresho ni pamoja na matumizi ya mikanda, ambapo Sheria ya sasa ya Usalama barabarani inasema ni kosa kisheria kwa dereva na abiria anayekaa kiti cha mbele kutokufunga mkanda wakati wa safari lakini sheria haisemi chochote kwa abiria wanaokaa viti vya nyuma. 

Alisema licha ya Kanuni za SUMATRA zinamtaka abiria yeyote kufunga mkanda ila kwa vile sheria mama (Road Traffic Act of 1973) ipo kimya katika eneo hilo utekelezaji wa kanuni hii unakuwa mgumu. 

Alisema eneo linguine ni pamoja na matumizi sahihi ya kofia ngumu, kwani Sheria ya sasa ya usalama barabarani inatambua kosa kwa mwendesha pikipiki kutokuvaa kofia ngumu lakini sheria hiyo haisemi chochote kwa abiria anayepanda katika chombo hicho wala kutaja aina na ubora wa kofia inayofaa.

“Kwa matumizi ya vilevi na uendeshaji vyombo vya usafiri: Sheria ya sasa ya usalama barabarani inasema kuwa itakuwa kosa kwa mtu yoyote kuendesha chombo cha moto akiwa na kiwango cha kilevi katika damu yake kinachozidi asilimia 0.08% katika mfumo wa mwili,

“Kiwango hiki ni kikubwa sana kikilinganishwa na tafiti zilizofanywa na Shirika la afya duniani na kupendekeza kiwango asilimia 0.05% kwa dereva aliyebobea na asilimia 0.02% kwa dereva mchanga. Hivyo basi ni rai yetu kuwa sheria ifanyiwe marekebisho ili iendane na kiwango cha sasa cha kimataifa kilichofanyiwa utafiti,” alisisitiza Bi. Sanga.

Aidha aliongeza kuwa adhabu zinazotolewa kwa sasa hazikidhi wala kuleta hofu kwa maderava wasiotaka kutii sheria na kanuni hivyo kuendelea kufifisha juhudi za kudhibiti tatizo la ajali za barabarani. 

“Mwendokasi umeendelea kuwa sababu kubwa ya ajali zinazogharimu uhai wa watu wengi. Sheria yetu inayo mapungufu kadhaa pamoja na juhudi nyingi za Jeshi la Polisi na wadau wengine kutaka kudhibiti jambo hili lemeendelea kuwa tatizo. Mfano Sheria ya usalama barabarani ya 1973 Kifungu cha 51(8) inatambua maeneo machache katika kuzuia mwendokasi, ni muhimu Sheria sasa itamke maeneo yote na si yale ya mjini tu au makazi, itamke wazi kuhusu maeneo ya shule, nyumba za ibada, maeneo ya michezo na mbuga za wanyama,” aliongeza Bi. Sanga katika taarifa hiyo.

Pamoja na mambo mengine, alisema sheria ya sasa ipo kimya juu ya suala la vizuizi vya watoto katika vyombo vya moto hasa kwa magari binafsi na tumeendelea kushuhudia madhara makubwa katika ajali zilizohusisha watoto vikiwemo vifo. 

Hata hivyo mtandao huo umewasihi wananchi kuwa na taadhari pindi watumiapo vyombo vya moto bila kujali mapungufu yaliyopo kwenye sheria za usalama barabarani ili kupunguza matukio ya ajali.

Kwa upande wake, Mwakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) usalama barabarani Mary Kessy, akitoa ufafanuzi kwa wanahabari, alibainisha takwimu zinaonyesha takribani watu milioni 1.25 duniani hufariki kila mwaka; huku nchini Tanzania asilimia 76 ya ajali za barabarani husababishwa na uzembe wa madereva, asilimia 8 ubovu wa barabara na ubovu wa vyombo vya moto kuchangia ajali hizo kwa asilimia 16.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Ifikapo 2020: Kupunguza vifo na ajali za barabarani kwa asilimia 50%”. Mtandao wa Wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya Sheria za Sera zihusuyo usalama barabarani Tanzania unaundwa na asasi zifuatazo;- TAWLA, TAMWA, WLAC, TCRF, TLS, TMF, RSA, AMEND TANZANIA, SHIVYAWATA, TABOA pamoja na SAFE SPEED FOUNDATION.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mabalozi wa Usalama Barabarani (RSA), John Seka akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa Kuwakumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani.Kushoto ni Isabela Nchimbi kutoka TAWLA na Bi. Edda Sanga wa TAMWA (kulia).


IGP SIRRO AKUTANA NA BALOZI WA CHINA

 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (kulia), akizungumza na balozi wa China nchini Mhe. Wang Ke, alipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo leo jijini Dar es salaam kwa lengo la kujitambulisha tangu alipoteuliwa kuwa Balozi hapa nchini. Picha na Jeshi la Polisi.
 Balozi wa  China nchini Mhe. Wang Ke, akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro (kulia), alipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya jeshi hilo leo jijini Dar es salaam kwa lengo la kujitambulisha tangu alipoteuliwa kuwa Balozi hapa nchini na kuahidi serikali ya nchi yake itaendelea kushirikiana na jeshi hilo. Picha na Jeshi la Polisi.


WAKAZI WA MKOA WA DAR ES SALAAM WAJITOKEZA KUPATA HUDUMA KATIKA MELI YA CHINA


MOI YAOKOA BILIONI 5 KWA KUPUNGUZA RUFAA ZA NJE YA NCHI.

Patrick Mvungi- MOI

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) imeokoa zaidi ya shilingi Bilioni 5 ambazo zingetumika kusafirisha wagonjwa nje ya nchi kufuata matibabu baada ya MOI kuanzisha huduma za kibingwa ambazo awali zilikua hazipatikani hapa nchini.

Hayo yamebainishwa katika ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya alipotembelea MOI na kukagua hali ya utoaji wa huduma, mazingira , miundombinu na kuwajulia hali wagonjwa pamoja na kukutana na menejimenti.

Akizungumza na menejimenti ya MOI, Dkt. Ulisubisya amepongeza kazi nzuri na kubwa inayofanywa ambayo imepelekea watanzania kupata huduma bora za kibingwa ambazo wangepaswa kuzifuata nje ya nchi.

“Mnafanya kazi nzuri sana, jambo ambalo linatupa faraja kubwa sisi viongozi wenu, naomba muongeze ubunifu zaidi, hamtakiwi kuifikiria MOI kwenye ukanda huu wa Afrika pekee bali duniani, hii ni changamoto kwetu sote kuifikisha hapo ”alisisistiza Dkt. Ulisubisya

Aidha, Dkt Ulisubisya amesema MOI imepunguza rufaa za kwenda nje ya nchi kwa asilimia 95% na asilimia 5% iliyobaki MOI inaweza kuimaliza kabisa na kusiwepo mgonjwa wa kwenda nje ya nchi.

Pia, amewaelekeza viongozi wa MOI kushirikiana na Wizara ya Afya kutafuta namna ya kufuta rufaa kwa kutoa mapendekezo na ushauri utakaosaidia kutatuliwa kwa changamoto hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya akizungumza na menejimenti ya MOI (hawapo pichani) katika ukumbi wa Mikutano wa MOI.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akimjulia hali mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji mkubwa wa mgongo, anayetoa ufafanuzi wa namna upasuaji huo ulivyofanyika ni Dkt. Nicephorus Rutabansibwa (Daktari bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mgongo). Kushoto ni Mganga mkuu wa Serikali Profesa Muhamed Kambi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya akikagua mashine mojawapo katika benki ya damu ya MOI.
Mtaalamu wa Maabara Bwana Mbuta Jackson akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya kuhusu namna benki mpya ya damu inavyofanya kazi kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa damu salama.


UKATILI DHIDI YA WANAWAKE TATIZO KUBWA HAPA NCHINI - DKT. NDUGULILE

Naibu Waziri wa Afya, Maendelego ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akitoa hotuba ya ufunguzi wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Dawati la Jinsia na Watoto linalosimamiwa na Jeshi la Polisi Tanzania.
Mkurugenzi wa CDF Koshuma Mtengeti akikabidhiwa cheti cha mdau wa Dawati la Jinsia aliyetukuka na Mhe. Naibu ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dr. Faustine Ndugulile.
Naibu Waziri wa Afya, Maendelego ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa Maendeleo mara baada ya kupokea vyeti kutoka Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Dawati la Jinsia na Watoto linalosimamiwa na Jeshi la hilo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendelego ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na Makamishina wa Jeshi la Polisi wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Dawati la Jinsia na Watoto linalosimamiwa na Jeshi la hilo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendelego ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile akipokea Maandamano ya Jeshi la Polisi wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Dawati la Jinsia na Watoto linalosimamiwa na Jeshi la hilo.

Na Anthony Ishengoma

Takwimu za shirika la Afya Duniani zinaoenesha kuwa asilimia 35 ya wanawake ulimwenguni ni wahanga wa vipigo na ukatili wa kingono au vyote kwa pamoja wakati hapa nchini Tanzania taarifa ya hali ya watu na Afya ya waka 2015 inaonesha kuwa asilimia 40 ya wanawake wenye umri kati ya miaka 15-49 wamefanyiwa ukatili wa kupigwa katika kipindi cha mwaka mmoja. Naibu Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Faustine Ndugulile amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano Mkuu wa wa mwaka wa Dawati la Jinsia na Watoto wa Jeshi la Polisi unaondealea kwa siku tatu.

Aidha Mhe. Ndugulile ameongeza kuwa pamoja na kuwepo ukatili wa kingono na vipigo kwa wanawake lakini pia vitendo vya ukeketaji bado ni tatizo kubwa hapa nchini akisema liko juu kwa kiwango cha asailimia 30 akiutaja mkoa wa Manyara kuwa na kiwango cha ukeketaji kwa asilimia 58. Aidha Mikoa mingine inayaoongoza kwa vitendo vya ukeketaji ni pamoja na Mkoa wa Dodoma kwa sailimia 47,Arusha asilimia 41 ikifutiwa na Mkoa wa Mara na Singida yenye kiwango cha asilimia 32.

Aidha ameonya kuwa ukatili wa kijinsia haukubaliki akitaja kuwa bado kuna kiwango kikubwa cha ukatili hapa Nchini na kinagharimu Jamii na Taifa letu katika Nyanja za kijamii, kisiasa na kiuchumi ikiwemo kuzorota kwa afya ya walengwa. Wakati huhuo Mwakilishi wa Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Kamishina wa Polisi Jamii hapa Nchini Mussa Ally Musa amesema kuwepo na ongezeko kubwa la taarifa za ukatili wa kijinsia na unyanyasaji kwa watoto tangu kuanzishwa kwa dawati hilo hapa Nchini ambapo kwa kipindi cha Januari-Desemba 2016 jeshi la polisi limepokea matukio 10,551 ya ukatili wa kijinsia kwa watoto ukilinganisha na matukio 9541 katika kipindi kama hicho 2015 na 2488 ya mwaka 2014.

Aidha ameitaja mikoa inayoongoza kwa matukio haya kuwa ni mkoa wa Moarogoro 1403, Rukwa 850, Singida 697,Iringa 649 na Dodoma kiwango cha matukio hayo ni 609 akiongeza kuwa kwa upande wa Tanzania visiwani Mikoa inayoongoza ni Mkoa wa Kusini pemba, Kusini unguja na Kasikazini unguja. Aidha kamishina Musa ameyataja makosa ya ubakaji kuwa ndiyo yanayoongoza ambapo Jeshi la Polisi mpaka sasa limepokea jumla ya matukio 4,423 ya ubakaji , shambulio 1,801 na shambulio la kudhuru mwili 1,021 na matukio yan kujerui 819.

Pamoja na ongezo hilo la matukio hayo pia dawati la jinsia la jeshi la polisi limekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ushirikiano mdogo kutoka kwa familia husika, uchache wa vifaa na majengo, uelewa mdogo wa wananchi na watendaji wa serikali pamija na ukosefu wa meaneo ya kuifadhi waanga wa ukatili.

Aidha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Faustine Ndugulile ameongeza kuwa changamoto inayokabili Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi ni ufinyu wa bajeti, upungufu wa rasilimali watu, akisema serikali itaendelea kufanyia kazi mapungufu yaliyoplo huku akitaja juhudi mojawapo ni uwepo wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.


Waziri Kairuki, Benki ya Dunia Wajadili Rasilimali Madini

Na Rhoda James, DSM

Waziri wa Madini Angellah Kairuki mwishoni mwa wiki alikutana na Ujumbe wa Benki ya Dunia jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufahamiana na kuangalia hatua mbalimbali zilizofikiwa katika utekelezaji wa Miradi ya Madini inayotekelezwa kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) unaofadhiliwa na Benki hiyo kwa kushirikiana na Serikali.

Pamoja na mambo mengine yaliyojadiliwa katika kikao hicho, Waziri Kairuki aliitaka Benki ya Dunia kuona namna ya kuwaendeleza Wataalam wa Sekta ya Madini ili kuwezesha uwepo wa Watalaam wa kutosha hususan katika masuala ya Uthaminishaji wa Madini ya Almasi, tanzanite na madini mengine ya vito na pia masuala ya uongezaji thamani madini kwa ujumla.

Pia, alishauri umuhimu wa kuboreshwa kwa Mtandao wa Huduma za Leseni kwa Njia ya Mtandao (Online Mining Cadastre) ikiwa ni pamoja na kuunganisha mtandao huo na Mamlaka nyingine ikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) ili taarifa zote zinazohusu madini na mapato yatokanayo na madini ziweze kupatikana kupitia mtandao huo.

Vilevile, aliishauri Benki hiyo kuhusu uuzwaji wa Madini ya Almas kwa njia ya Mnada kama vile inavyofanyika kwa Madini ya Tanzanite, lengo likiwa ni kuwezesha Serikali kunufaika na madini hayo. Aliongeza kuwa, baada ya Serikali ya Tanzania kupitisha Marekebisho ya Sheria ya Madini kupitia Sheria ijulikanayo kama (The written laws (Miscellaneous Amendements) Act, 2017), alisema kuwa, baadhi ya wawekezaji wameonesha wasiwasi kuhusu marekebisho hayo.

Hivyo, Waziri Kairuki amewataka wawekezaji kutokuwa na hofu kwani mabadiliko hayo yanalenga kuhakikisha kuwa Serikali inanufaika ipasavyo kutokana na rasilimali zake za madini. Aidha, alisema kwamba, nia ya Serikali kuhusu kuvutia wawekezaji iko palepale ilimradi wazingatie Sheria na taratibu. Vilevile, Waziri Kairuki alieleza kwamba, ni vema Benki ya Dunia ikaangalia namna bora ya kuhakikisha madini yote ya Tanzanite yanayouzwa nje ya nchi yanakuwa na Hati ya Uhalisia inayoonyesha chanzo cha madini hayo suala ambalo litawezesha Taifa kupata mapato stahiki kutokana na rasilimali hiyo.

Vievile, Waziri Kairuki alizungumzia suala la udhibiti wa utoroshaji madini na kusisitiza kuhusu kuwepo na namna bora ya kuzuia utoroshwaji wa madini ya Tanzanite ikiwemo kujulikana kwa idadi ya wachimbaji wadogo, wa kati, kiasi kinachopatikana na mahali madini hayo yanapouzwa. Pia, Waziri Kairuki aliishukuru Benki ya Dunia kutokana na ushirikiano ambao umekuwepo baina ya Serikali kwa kipindi chote na kueleza kuwa, Serikali iko tayari kutekeleza miradi husika kikamilifu kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI


Rais Magufuli hajatengua utengua uteuzi wa Dkt. Laurian NdumbaroWAZIRI KALEMANI AKUTANA NA BALOZI WA MAREKANI, INDIA NCHINI

Leo tarehe 20 Novemba, 2017, Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amekutana na Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Inmi Patterson na Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya kwenye Ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo jijini Dar es Salaam. Lengo la ziara ya mabalozi hao lilikuwa ni kufahamiana na kujadili namna ya kushirikiana katika miradi ya nishati nchini.

Akizungumza na Balozi wa Marekani Nchini Dkt. Inmi Patterson aliyeambatana na wawakilishi kutoka Shirika la Misaada la Marekani (USAID), Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) na Mradi wa Power Africa uliopo chini ya MCC, Dkt. Kalemani alielezea mikakati ya Serikali ya kuhakikisha nishati ya uhakika inapatikana nchini kuwa ni pamoja na mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za maji wa Stieglers Gorge uliopo Rufiji mkoani Pwani, miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi ya Kinyerezi I, Kinyerezi II na Kinyerezi III na miradi ya nishati jadidifu kama vile upepo, jua na jotoardhi.

Dkt, Kalemani alisema Serikali kupitia Wizara ya Nishati imeweka malengo ya kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 kiasi cha Megawati 5000 za umeme zinazalishwa na vijiji vyote nchini kupata nishati ya umeme wa uhakika na kwa gharama nafuu. Waziri Kalemani alitumia fursa hiyo kualika wawekezaji kutoka Marekani kuwekeza kwenye sekta ya nishati ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa malengo ya Wizara ya kuhakikisha nishati inachangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi. Naye Balozi wa Marekani Nchini, Dkt. Inmi Patterson alipongeza mikakati mizuri ya Wizara katika kuhakikisha nishati ya uhakika inapatikana kwani pasipo umeme wa uhakika hakuna maendeleo yoyote.

Balozi Patterson alimhakikishia Waziri Kalemani kuwa nchi ya Marekani ipo tayari kushirikiana na nchi ya Tanzania hususan katika sekta ya nishati pamoja na sekta nyingine ili kuchochea kasi ya maendeleo nchini. Wakati huo huo Waziri Kalemani akizungumza na Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya aliyemtembelea ofisini kwake mbali na kueleza mipango ya serikali katika kuhakikisha nishati ya uhakika inapatikana, aliomba nchi ya India kusaidia kupitia wataalam wake kushirikiana na wataalam wa Tanzania katika sekta ya nishati kutokana na kuwa na uzoefu mkubwa.

Aliendelea kusema kuwa Tanzania imekuwa na historia ndefu ya ushirikiano na kusisitiza kuwa umefika wakati wa kuboresha ushirikiano katika sekta nyeti ili uchumi wa nchi uweze kukua kwa kasi na Serikali kutimiza Dira ya Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2025 yenye kufafanua kuwa nchi kuingia kwenye orodha ya nchi zenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 kupitia uboreshaji wa huduma za jamii.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kulia) akisalimiana na Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Wizara ya Nishati zilizopo jijini Dar es Salaam.


DR NTUYABALIWE FOUNDATION YAHAMASISHA WANAFUNZI KUJIAMINI NA KUSOMA KWA BIDII

Wanafunzi wamehamasishwa kujiamini na kusoma kwa bidii ili kujijengea msingi imara ya mafanikio katika maisha yao.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Muasisi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Bi. Jacquiline Mengi alipowatembelea wanafunzi wa shule za msingi za Muungano na Serengeti zilizopo Manispaa ya Temeke, siku  ambayo duniani kote inaadhimishwa siku ya mtoto Duniani.
Akizungumza na wanafunzi hao Muasisi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation amesema ujumbe wake muhimu kwao wakati wa kuadhimisha siku ya mtoto Duniani ni kujiamini na kusoma kwa bidii, kwani ndiyo ufunguo wa mafanikio katika maisha
Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Huduma ya simu kwa Mtoto ( C-SEMA)  Bw. Michael Marwa amewataka watoto kuripoti mara moja kwa njia ya simu vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto ili wahusika wachukuliwe hatua.
Akitoa shukrani Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Muungano, Esther Matowo amesema ujio wa Muasisi wa Taasisi ya Dr Ntubaliwe umewahamasisha  wanafunzi kujitambua na kujua wajibu wao. 
Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Salum Upunda, Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Serengeti Daud Sabai na walimu wa shule hizo mbili.
Mkurugenzi wa Dr.Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akizungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi ya Muungano na Serengeti alipowatembelea katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto Duniani yanayofanyika Novemba 20 ya kila mwaka.
Mkurugenzi wa Huduma ya simu kwa Watoto( C-SEMA)  Bw. Michael Marwa akionesha namba ya huduma zinazotumika kuripoti mara moja kwa njia ya simu vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto ili wahusika wachukuliwe hatua wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto Duniani yanayofanyika Novemba 20 ya kila mwaka yaliyofanyika katika shuleni hapo.
Afisa Elimu na Ufundi manispaa ya Temeke, Salum B. Upunda aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya watoto Duniani mara ya viongozi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation walipotembelea shuleni hapo leo.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Muungano, Esther Matowo akitoa shukrani kwa uongozi wa Dr.Ntuyabaliwe Foundation kutembelea shuleni hapo na kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto Duniani.
Mkurugenzi wa Dr.Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi ya Serengeti na Muungano mara baada ya kuzungumza na wanafunzi hao wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto Duniani.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


WATAKWIMU WATAKIWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YA KISASA KATIKA UKUSANYAJI WA TAKWIMU BORA

 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Alibina Chuwa akisisitiza jambo wakati wa hafla ya maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Barani Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu Bw. Irenius Ruyobya, Mwakilishi wa Gavana wa Benki Kuu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchumi wa benki hiyo Bw. Johnson Nyera, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Watakwimu Tanzania (TASTA) na Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Abdalah Ramadhan Abeid. Kauli mbiu ya mwaka huu ni " Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora".
 Mwakilishi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchumi wa benki hiyo Bw. Johnson Nyera akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Takwimu barani Afrika iliyofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mwl. Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei Bibi. Ruth Minja na Mwakilishi wa Asasi za Kiraia Bw. Stephen Chacha. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni "Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora".
 Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Abdalah Ramadhan Abeid akitoa neno la shukrani  katika hafla ya maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Barani Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwakilishi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchumi wa Benki hiyo Bw. Johnson Nyera, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Alibina Chuwa na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Watakwimu Tanzania (TASTA.) Bibi. Yasinta Kijuu. Kauli mbiu ya mwaka huu ni " Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora".
 Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Bibi. Elizabeth Talbert akizungumza katika hafla ya maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Barani Afrika leo Jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya mwaka huu ni " Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora".
 Mwanafuzni wa Kidato cha Tano kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana Kisutu Bi. Felister Mande akipongezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Alibina Chuwa baada ya kuwa mshindi wa pili katika shindano la insha kuhusu kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika mwaka huu inayosema " Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora".Kutoka kulia ni Mwakilishi wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchumi wa hiyo Bw. Johnson Nyera, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Watakwimu Tanzania (TASTA.) Bibi. Yasinta Kijuu, Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Abdalah Ramadhan Abeid na Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu Bw. Irenius Ruyobya.
 Mwanafuzni wa Kidato cha Tano kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana Kisutu Bi. Edda Magesa akipokea zawadi ya shilingi laki tatu kutoka kwa mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Uchumi wa BoT Bw. Johnson Nyera baada ya kuwa mshindi wa kwanza katika shindano la insha kuhusu kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika mwaka huu inayosema " Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora".Kutoka kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Alibina Chuwa Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Watakwimu Tanzania (TASTA.) Bibi. Yasinta Kijuu, Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Abdalah Ramadhan Abeid na Mkurugenzi wa Shughuli za Kitakwimu Bw. Irenius Ruyobya.
 Mgeni rasmi wa katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchumi toka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bw. Johnson Nyera akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi kutoka Shule za Sekondari Kisutu Wasichana na Azania walioshiriki shindano la insha kuhusu kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika mwaka huu inayosema " Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora" wakati wa maadhimisho hayo leo Jijini Dar es Salaam.  Wanafunzi kutoka kushoto ni Edda Magesa (mshindi wa kwanza), Fred Komba (mshindi wa tatu) na Felister Mande (mshindi wa nne).(Picha na: Frank Shija - MAELEZO)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Wabunge wawapongeza NSSF, PPF na magereza mradi wa kiwanda cha sukari cha Morogoro

KAMATI ya Bunge ya Katiba na Sheria imepongeza namna mifuko ya hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF inavyotekeleza mradi wa pamoja wa ujenzi wa kiwanda cha sukari unaofahamika kama Mkulazi huku ikitoa wito kwa wadau hao kuhakikisha wanakamilisha mradi huo kwa wakati ili kulinusuru taifa na uhaba wa bidhaa hiyo.

Mwisho mwa wiki kamati hiyo ilitembelea mradi huo unaotekelezwa katika gereza la Mbigiri, lililopo Dakawa mkoani Morogoro kupitia kampuni Hodhi ya Mkulazi Holding inayoshirikiana na Jeshi la Magereza nchini.

"Baada ya kusikiliza mpango mikakati na kisha kutembelea shamba husika kiukweli kamati yetu imeridhishwa sana na jinsi wadau hawa wanavyotekeleza mradi huu. Ni wazi kuwa walifanya utafiti wa kutosha kabla na matunda yake kiukweli yameanza kuonekana kikubwa tu tunachowaomba wamalize mradi huu kwa wakati .'' alisisitiza  Mwenyekiti wa kamati hiyo Bw Mohamedi Mchengelwa.

Aidha, wajumbe wa kamati hiyo walionyesha kuridhiswa zaidi na namna mradi huo unavyohusisha wananchi walio jirani na maeneo ya mradi ambao mbali na kupata ajira za moja kwa moja pia wamepatiwa fursa ya kulima miwa ili kukiuzia kiwanda hicho, hatua waliyosema kuwa itapunguza tatizo la ajira na kuongeza kipato cha wananchi.

"Kingine kikubwa zaidi kwa wadau hawa ni kuhakikisha kuwa mradi huu hauishii kwenye kuzalisha sukari tu bali pia bidhaa zitokanazo na mabaki ya malighafi za miwa ikiwemo ethanol, vyakula vya mifugo pamoja na uzalishaji wa nishati umeme,'' alisema mjumbe Selemani Zedi huku akiungwa mkono na wenzie akiwemo Mbunge wa Wawi Ali Salehe.
 Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama  (wa tatu kulia) akiwaongoza baadhi ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria  kukagua shamba hilo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria Bw Mohamedi Mchengelwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua shamba kubwa la miwa lililopo katika gereza la Mbigiri lililopo Dakawa mkoani Morogoro ambalo ni sehemu ya mradi wa ujenzi wa kiwanda cha sukari kinachojengwa kwa ubia kati ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF, PPF na jeshi la Magereza nchini.
 Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua shamba hilo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mkulazi ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius Kahyarara akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua shamba hilo. Kwa mujibu wa Prof. Kahyarara hadi kufikia mwishoni mwa mwaka ujao mradi huo utakuwa tayari umeanza kuzalisha sukari pamoja na baadhi ya bidhaa ambatanishi ikiwemo uzalishaji wa umeme.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA