Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

WATUMIAJI wa Simu na mitandao wameaswa kuwa waangalifu katika kujiepusha na matepeli wanaotumia mitandao hiyo katika kujipatia kipato.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Mawasiliano kwa Umma, Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Semu Mwakyanjala amesema kuwa simu na mitandao inatakiwa kutumika kwa uangalifu zaidi ili mawasiliano yawe na tija kwa mtumiaji.

Amesema wizi katika mitandao umkeuwa ukifanyika kila siku,hivyo kila mtu akiona taarifa tofauti anatakiwa kuripoti katika vyombo vya dola ili wizi huo usiweze kufanyika na mtu anayefanya hivyo kuanza kufuatiliwa.

Mwakyanjala amesema TCRA inafanya uchambuzi wa taarifa za matukio ya usalama wa mitandao kutoka katika vyanzo mbalimbali vya nchini , kimataifa na matokeo ya uchambuzi huo kuongeza usalama wa matumizi ya mawasialiano ya simu, komputa pamoja na Internet.

Aidha amesema TCRA inafanya tathimini ya udhaifu wa mifumo ya komputa ya mitandao ya wadau wake isiweze kusambaza ujumbe wa chuki maudhi au uchochezi unapotokea kwa mtu mwingine na kinachotakiwa kufanyika ni kufuta pale aunapoona taarifa haikidhi vigezo katika mawasiliano.
Kaimu Meneja Mawasiliano kwa Umma, Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Semu Mwakyanjala akizungumza na waandishi wa habari juu ya mamlaka hiyo inavyofanya kazi leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa habari wa idara ya habari MAELEZO, Fatma Salum.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...